Habari Mange,
Mimi ni mfuatiliaji wa Blog yako, na nimewahi kuleta issue yangu nikapewa ushauri poa tu.
Wakati huu sio kuhusu mimi, ila kuhusu mtoto ambaye nimekutana naye.
Ninaishi kanda ya ziwa na hapa jirani yangu kuna binti mmoja who is in her late 11th. Huyu binti ambaye sitamtaja jina anaishi na bibi yake, dada na mama mdogo. mama yake ameolewa sehemu nyingine. Kwa sasa yuko darasa la tatu (mabinti wa huku at times wanachelewa kuanza shule) though ameacha kutokana na shida yake.
Story yenyewe iko hivi!
Huyu binti na familia yake huwa wanachota maji nyumba ya jirani (maji ya kununua kwa ndoo). Siku moja alipoenda kuchota maji, kijana muuza maji alimwambia chenji ufuate baadaye, binti alipofuata chenji, kijana akamkaba, akambaka. Hiyo ni almost ten months ago. Binti akarudi nyumbani anatoka damu akamweleza dada yake, dada akamwambia kaoge, then wakamweleza bibi na bibi akemweleza mama. mama akaenda kwa kijana akagomba tu, then yakaisha.
Binti alipoenda kuchota maji siku ingine, kijana akamtukana kuwa amemweleza mama yake, na akamwambia kuwa atamshika tena. Binti hakusema kwa yeyote, maisha yakaendelea.
Miezi michache baadaye, yule binti akiwa amekwenda kuchota maji, yule kijana akamshika binti, akamsukuma ndani, akambaka tena. This time baada ya kumbaka alimpiga akamfukuza. (Katika mara zote hizi mbili, kijana amekuwa akimtishia kumuua endapo atapiga kelele)
Binti aliporudi nyumbani akamweleza dada yake kwa kuwa bibi yao hakuwepo, dada akamwambia akaoge. Walipomweleza mama yao, mama hakuchukua hatua yoyote. Bibi aliporudi akaelezwa, bibi naye akakaa kimya.
Sasa Mange mbaya ni kuwa yule binti kapata ujauzito. As i am writting this email, she is FIVE MONTHS PREGNANT. Anaeleza kuwa alivunja ungo mara ya kwanza na mwezi huo huo ndo alipobakwa na kupata ujauzito. Ni mdogo sana! hajaweza hata kujisafisha mwenyewe akatakata, now she will have to wash her own baby soon!
Mama yake ameambiwa lakini mpaka leo hajafika anapoishi binti yake anadai kuwa yuko busy. Mpaka sasa hivi hakuna aliyekwenda polisi, na kijana aliyembaka amekimbia! Na ni kijana ambaye yuko mid 20s
I talked to the girl, she have one wish ANATAKA KUENDELEA NA SHULE COZ SHE WANTS TO BE A DOCTOR! How sad!!
Nimelileta, just to share how evil some men can be!
3 comments:
jaman huyo anafaa kufungwa maisha yake kwa unyama alio mfanyia mtoto huyo
jamani ni ukatili wa waina gani huu jamani, na huyo mama ni kunogewa gani huko anakonogewa mpaka anaona mwanae sio wa muhimu jamani? mie nakushauri please mpenzi kama unaweza kumsaidia kampime kwanza HIV na magonjwa ya sinaa thn kama una uwezo msaidie mpaka ajifungue ikiwezekana hata ukaishi nae kwako mtoto akikuwa amrudishe kwao thn wewe umuendeleze au umpeleke kwa wahisani.. mpe pole sana jamani
Mchango upite AMTTA fasta
Post a Comment