Friday, October 28, 2011

MTOTO HUSSEIN RISASI ANATAFUTWA

Familia ya Bw Alhaj Abdul Risasi wa Kawe jijini Dar es Salaam inatangaza kupotelewa na mtoto wao Hussein Risasi (15) anayesoma shule ya Msingi Olympio iliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Alhaj Risasi ni kwamba Hussein alitoweka nyumbani kwao Kawe jijini Dar es Salaam Ocktoba 25 mwaka huu mara baada ya kurejea akitokea shuleni.
Kabla ya tukio hilo Hussein alianza utoro wa kwenda shule kwa madai kwamba amekuwa haelewi anachofundishwa na walimu wake na kwamba wanafunzi wenzake wamekuwa wakimcheka  kitendo ambacho hakukipenda.
Akifafanua  zaidi Alhaj Risasi amesema kuwa, kutokana na tabia hiyo ya utoro aliyoianza Hussein ambaye ni pacha na Hassan Risasi anayesoma Nairobi, alimwita na kumkanya kutokana na vitendo hivyo.
Hussein amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya athma tangu utoto wake jambo linaloathiri pia afya yake mara kwa mara.
Kwa yeyote atakayemuona anaombwa kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi nchini au kupitia namba za simu 0715  611 277, 0713  314  442  au 0787 377 822.

Wednesday, October 26, 2011

BI KIDUDE BADO YUPO YUPO

Jana kwenye mtandao wa Facebook ulitokea uvumi kwamba Bi Kidude amefariki na leo habari hizi zimeweza kukanushwa na I-view Media kwa kutuwekea picha hii katika mtando huo huo.

Hivi inakuwaje mtu anazushiwa kifo?

WE LOVE U BI KIDUDE MUNGU AZIDI KUKUBARIKI

MWEI YATOA MKOPO NEWALA ,MTWARA

Wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa  kijij cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,wakiwa wameketi wakisubiri kupatiwa mkopo wa fedha taslimu unaotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini bila riba.
Meneja wa Vodacom Tanzania  wa  Mradi wa  MWEI Mwamvua Mlangwa  akimpatia Mwanaidi  Musa  mkopo wa fedha taslimu   kwa ajili ya kufanyia biashara zake na kuzirudisha fedha hizo bila riba yoyote,aliyekaa kushoto ni Mratibu wa Mfuko huo Ally Mbuyu.
Wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa  kijij cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,wakimsikiliza Meneja wa Vodacom Tanzania  wa  Mradi wa  MWEI Mwamvua Mlangwa hayupo pichani ,wakati  wakisubiri kupatiwa mikopo yao ya  fedha taslimu zinazotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini bila riba.
Meneja wa Vodacom Tanzania  wa  Mradi wa  MWEI Mwamvua Mlangwa  akiongea na wakinamama wajasiriamali wadogowadogo wa  kijij cha Kitangari Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara,kabla ya kuanza kuwapatia  mikopo ya fedha taslimu zinazotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake  wa MWEI unaowakopesha wakina mama hapa nchini na kurudisha fedha hizo bila riba.  

8020 FASHIONS 5TH ANNIVERSARY

NI JUMAPILI HII TAREHE 30 OCTOBER 2011
KIINGILIO 30,000/= 
 DIAMOND JUBILEE
C U THERE!

MALKIA WA MIPASHO KHADIJA KOPA NDANI YA UK TAYARI KWA MAKAMUZI...!!!




Malkia wa mipasho Bi. Khadija Kopa ameingia leo jijini London akitokea Dar Es Salaam tayari kwaajili ya onyesho lake litakalofanyika Milton Keynes siku ya Jumamosi 29th October 2011 katika ukumbi wa The Golden Lounge, Unit 35 Baton Rd, Milton Keynes, MK2 3LH.

Akizungumza na mwadishi wa blog ya TZ-ONE ya UK Bw. Ally Muhdin, Malkia wa mipasho aliwaahidi wapenzi wake kuwa atawafurahisha na kuhakikisha wataburudika na nyimbo zake mpya na zile za zamani.

Vilevile kampuni ya African Splash promotions pamoja na Infinity Entertainment wamewaomba wapenzi wote wa Khadija Kopa kujitokeza kwa wingi kwenye ukumbi wa The Golden Lounge, Milton Keynes kwaajili ya kuweza kumuona mwanamuziki huyo.

Tuesday, October 25, 2011

SITAKIII AGEUKEEE....KIM KARDASHIAN.....

                                                        KIATUU + KIAKALIO=KIKOTI

KIMEMWAGAAA KIJASHOOO NDANI YA TANDIKO JEKUNDU......KELLY OSBOURNE

                                                        AFYAAAAA IMEZIDII LOL

MWANAMKEE KITUNEEEE....SIO KILALEEEEE..SALMA HAYEK

                                                                  DOOOOH
                         INAITWA FULL PACKAGE ...KIFUA,KIUNO NA ULEGGGGGG       

Monday, October 24, 2011

SHANIIIIIII J4......KIMODEL ZAIDIIIII...LOVE UUUUUU DOGO

                                                     HAWWWWT XXX
                                                       GAWWWWWJUS X
                                                 MASHALLLAH
                                                  SANTAAAAA XXXX
                                                 
                                                 MI LOVE DIS AWWWW

                                                     TOP MODELLLLLLLL
                                                      ASHHHHHHHHHHH
                                           
                                                                HOTO HOTOOOOOOOOO

                                                              YALLLAH
                                                   KIMODELLLLLL HASAAA XX

                                                        AMENOGAJEEEE
                                                  BLACK BEAUTYYYYYY

SHUKRANI KUTOKA KWA MISS JESTINA GEORGE BLOG

SALAM,
Napenda kutoa shukurani zangu za pekee kwa Mwenyezi Mungu, Familia yangu, Marafiki zangu, mashabiki wangu, wadau na watanzania wote kwa ujumla walioweza kunipigia kura ambazo zimefanikisha blog ya MissJestinaGeorge kuibuka kidedea na kunyakua ushindi mkubwa wa kuwa ''BLOG BORA YA MWAKA 2011''  katika tuzo za BEFFTA zilizofanyika nchini UK mapema wiki iliyopita.
 
Mchakato mzima wa kumtafuta mshindi ulikuwa na changamoto lukuki ukizingatia ya kwamba kulikuwa na jumla ya blogs 15 za kimataifa kutoka nchi mbali mbali Duniani. Kutokana  na ushirikiano wenu mzuri  mmeiwezesha blogu yetu kupata ushindi mnono na vile vile kunipatia fursa nzuri ya kuiwakilisha vyema Tanzania Ughaibuni.

Ni vigumu kumshukuru kila mtu mmoja mmoja kwa mchango wenu uliosadia kuwezesha blog yetu kunyakua ushindi mkubwa ingawa ningependa kuwatambua wafuatao: kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu zote za dhati kwa  timu yaURBAN PULSE CREATIVE  kwa mchango wao mkubwa waliotoa, wanachama wenzangu wa AMTTA (Amka Mwanamke Twende Tujikomboe Afrika) kwa kuwa na mimi bega kwa bega nawapenda sana. Pia natoa shukrani kwa Bloggers wenzangu wote, tovuti mbalimbali, TONE RADIO popote pale walipo kwa michango yenu. 

Nawasihi sana tuendelee kushikamana, kupendana na Kusaidiana kwa hali na mali ili isiwe tu kuleta maendeleo nchini kwetubali pia kupeperusha bendera ya nchi yetu Tanzania Duniani kote.

Napenda kuitoa wakfu tuzo hii kwa dada yangu mpendwa Kissa George aliyetutoka ''I miss you so much Sis'' najua kama angekuwa hai angefurahia sana.
 
Mwisho namshukuru sana binti yangu Iman ambae amekuwa nguzo na muhumili mkubwa katika maisha yangu kwa kunipatia nguvu za kuendelea mbele siku hadi siku.

Binadamu kushukuru ni wito ila leo umekuwa ni wajibu wangu.
 
Asanteni sana,
 
Mungu awabariki sana na ninawapenda sana
Jestina George


HAPPY BDAY ASHURA SOMO.....ASHLEY SOMO SOMO......AMTTA PENDA WEYEEE KICHUNAAA XXXXX

                                                     MAN U...ASHHHHHHHHHH,,,OYEEEE XXX POLEE

Sunday, October 23, 2011

TWINS WA MARIAH CAREY AND NICK CANNON ...........WAMENOGAJEEE

                                                  LA FAMILY
                                                        MOROCCAN AND MANROE CANNON

                                                             MARIAH CAREY......ULEZIIIIII

BLOG YA MWANACHAMA WA AMTTA MISS JESTINA BLOG YASHINDA TUZO YA BLOG YA MWAKA UK...!!!

Jestina akiwa amevalia vazi liliobuniwa na KIKI wa Kiki's Fashion Tanzania
Jestina akienda kupokea tuzo baada ya kutangazwa Blog of the year
Jestina akimwaga speech kuwashukuru wote waliompigia kura na kumsupport
Zulfa, Jestina, Lynn & Frank kutoka Urban Pulse wakifurahia ushindi
Jestina akiwa na mdogo wake Luiza baada ya kupokea tuzo
Jestina akiwa na marafiki zake waliokwenda kumsupport kutoka kushoto Jacque Maina, Jestina, See Li, Amina & Zulfa musa
Frank Eyembe kutoka Urban Pulse, Lynn Kapinga, Jestina George, Mashel & Musa Sissasi Sarr

Jestina akiwa katika pose na Tuzo yake
*******************
Salam,

Urban Pulse Creative inapenda Kumpongeza dada yetu Jestina George kwa kushinda tuzo muhimu ya Blog ya Mwaka  katika  tuzo za BEFFTA zilizizofanyika Jumamosi tarehe 22 Octoba 2011 ndani ya ukumbi wa Lighthouse, Camberwell jijini London.

Wakati akitoa Hotuba yake Jestina alianza kwa kumshuru Mungu ambae amemwezesha kumpatia uzima, afya njema pamoja na mafanikio  makubwa aliyopata mwaka huu.  Aliendelea kwa kuwashukuru Wazazi wake na mwisho wadau wote ambao walimpigia kura Pia Mabloggers na Tovuti mbalimbali ambazo zimemsaidia kumpigia debe na kuibuka mshindi wa BLOG OF THE YEAR 2011 kutoka kwenye kundi lenye Blog 15 za kimataifa. Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kuingia, kushinda na kumfanya kuwa Mtanzania wa Kwanza kupokea tuzo za BEFFTA  kwa upande wa Blogs

Jestina George ameitoa wakfu Tuzo yake kwa dada yake mpendwa Kissa George ambaye hatunaye tena hapa Duniani.

Vazi lake lilibuniwa na KIKI wa Kiki's Fashion Tanzania. Kwa maelezo zaidi na taswira mbalimbali za tukio hili Tembelea http://missjestinageorge.blogspot.com/

Asanteni,

Urban Pulse Creative
**********************
HONGERA SANA MAMA MEDIA WA AMTTA WE'RE VERY PROUD OF YOU & WE LOVE YOU. AMTTA JUU SANA.

ARSENAL 3-STOKE1.......ARSENAL UWIIIIIIIIIIIIIII AIIIIIII

                                                         GERVINHO.....ACHACHAAAAAAA
                                                    
                                                   VAN PERSIE
                                                      WENGERRRRRRRRRRRR
                                                                HHHHAAAA MZAIREEEE

MAN UUUUUUUUUUUUUUUUUU...SHIIISHHH .....AIIIII....MAN CITYYYYYYYYYY

                                                    UBAOOOOO HUOOO
                                                     POOOOOOZI ....AU VIUNOO HOI
                                                 MAN CITY KAZINI.....
                                                 BABA MPIRA UMEKWISHAAA ALAAA
                                                      MTUUU MZIMAA KASHIKISHWA UKUTAAAA....TEHEEE